Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Rais Uhuru Kenyatta walipokutana katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dubai waliposimama kwa muda wakiwa njiani kuelekea nyumbani wakitokea Washington DC, Marekani, walikohudhuria Mkutano wa Marekani na Wakuu wa nchi wa Afrika ulioandaliwa na Rais Barack Obama.
Mama Salma Kikwete akisalimiana na Rais Uhuru Kenyatta walipokutana katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dubai waliposimama kwa muda wakiwa njiani kuelekea nyumbani wakitokea Washington DC, Marekani, walikohudhuria Mkutano wa Marekani na Wakuu wa nchi wa Afrika ulioandaliwa na Rais Barack Obama. Kulia ni Balozi Mdogo wa Tanzania, Dubai, Mhe Omari Mjenga.
Balozi wa Tanzania katika Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE), Mhe. Mbarouk Nassor Mbarouk akiwa na balozi wa Kenya katika UAE Mhe. Mohamed Gello katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dubai ambapo mabalozi hawa walifika kuwapokea Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Rais Uhuru Kenyatta waliosimama kwa muda mjini hapo wakitokea Washington DC, Marekani, walikohudhuria mkutano wa Marekani na Wakuu wa nchi za Afrika ulioandaliwa na Rais BArack Obama wa Marekani.(Picha na IKULU)
No comments:
Post a Comment