Friday, August 15, 2014

HALI YA AFANDE SELE SI NZURI BAADA YA KUFIWA NA MAMA WA WATOTO WAKE


Msanii wa Bongo Fleva,Afande Sele hali yake imekuwa mbaya baada ya kufiwa na mzazi mwenziye Asha Mohamed’Mama Tunda’.Msanii huyo inawezekana akawa ni moja kati ya watu maarufu hapa nchini ambao wanaongoza kwa kuwataja wenza wao sehemu tofauti tofauti ambapo zaidi ya miaka 10 amesikika akimtaja wa ubavu wake, mara kwa mara hiyo ni wakati wakiwa wanaishi pamoja na mama tunda ambaye ni mzazi mwenzake waliyezaa nae watoto wawili, wa kwanza ni Tunda pamoja na Asante Sanaa. Mama Tunda amefariki dunia usiku wa kuamkia leo, na kabla ya kifo chake alikuwa anasumbuliwa na maradhi ya malaria pamoja na pumu, mazishi ni leo saa tisa mchana,hata hivyo clouds fm imezungumza na msanii wa karibu wa Afande Sele,MC Koba baada ya Afande Sele kushindwa kuzungumza kutokana na hali yake kuwa mbaya.




No comments:

Post a Comment