Mshauri
wa Kimataifa wa Kujitegemea, James Rugemalira (kulia), akimtambulisha
kwa madaktari (hawapo pichani), Daktari Bingwa wa magonjwa ya saratani
ya matiti, Profesa Anthony Pais, kutoka Bangorole India, Dar es Salaam
jana. Daktari huyo kesho jioni anatarajia kufanya mhadhara na madaktari
wa Kitanzania na wadau wa sekta ya afya kujadili ugonjwa huo katika
Hoteli ya Protea Court Yard. Daktari huyo yupo nchini kwa mwaliko
maalumu wa mshauri huyo wa Kimataifa.
Mshauri
wa Kimataifa wa Kujitegemea, James Rugemalira (kulia), akiwa na daktari
huyo (katikati), Kushototo ni Mama Benedicta Rugemalira. (Imeandaliwa
na mtandao wa www.habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)
Profesa Anthony Pais (katikati), akizungumza na madaktari wa Tanzania. Kushoto ni Dk.Maleare na Dk. Fredy
Profesa Anthony Pais (kulia), akizungumza na madaktari wa Tanzania.
Wadau
wa sekta ya Afya wakiagana na daktari huyo nyumbani kwa Mshauri wa
Kujitegemea wa Kimataifa, James Rugemalira Makongo Juu jijini Dar es
Salaam.
Dar es Salaam, Tanzania
DAKTARI Bingwa wa ugonjwa wa saratani ya matiti ,
Profesa Anthony Pais, kutoka Bangorole nchini India kesho Agosti 28, 2014 anatarajia kutoa muhadhara kuhusu ugonjwa
huo.
Akizungumza na Mtandao wa www.habari za jamii.com. Dar es Salaam leo
Mshauri wa Kimataifa wa Kujitegemea, James Rugemalira alisema ujio wa daktari
huyo hapa nchini ni fursa kwa watanzania kutokana na changamoto kubwa iliyopo
kuhusu ugonjwa huo.
"Daktari huyu amebobea katika ugonjwa wa
saratani ya matiti na amefanya operesheni nyingi za ugonjwa huo ni wakati mzuri
kwetu kwenda kumsikiliza kesho jioni Hoteli ya Protea Court Yard" alisema Rugemalira.
Alisema kesho daktari huyo atatoa mhadhara kwa
madaktari wa kitanzania na wadau wa sekta ya afya kuhusu ugonjwa huo na jinsi
ya kukabiliana nao.
Rugemalira alisema daktari huyo atakuwepo nchini
kwa siku kadhaa na leo alitembea Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Taasisi ya
Kansa ya Ocean Road na Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH).
Daktari huyo yupo nchini kwa mwaliko maalumu wa
mshauri huyo wa kimataifa ili kuona namna ya kusaidia tatizo hilo.
No comments:
Post a Comment